Psalms 78:55-58

55 aAliyafukuza mataifa mbele yao,
na kuwagawia nchi zao kama urithi,
aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.

56Lakini wao walimjaribu Mungu,
na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,
wala hawakuzishika sheria zake.
57 bKama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,
wakawa wasioweza kutegemewa
kama upinde wenye kasoro.
58 cWakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,
wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.
Copyright information for SwhNEN